Leo April 12, 2017 nimekutana na stori ambayo inaihusu World Economic Forum kutoa list ya nchi zenye usalama zaidi duniani ambapo katika taarifa iliyochapishwa na mtandao wa The Telegraph April 11, 2017 nchi ya Finland imetajwa kuwa namba moja kwa kuwa na usalama zaidi duniani huku nchi zenye historia ya vita kama Rwanda, Oman na United Arab Emirate zikiingia kwenye Top Ten mwaka 2017.
Aidha, katika list hiyo pia zimetajwa nchi zisizo na usalama duniani ambapo barani Afrika nchi za Kenya, Ethopia, DR Congo na Mali zimetajwa kama nchi zenye viashiria vya vurugu na zisizo na usalama ambapo kwa mujibu wa World Economic Forum, nchi hizi hupata watalii wachache kwa mwaka ukilinganisha na nchi nyingine.
No comments:
Post a Comment