Baba wa kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba, Fassou amefariki dunia Ijumaa usiku akiwa na umri wa miaka 79.
Fassou Antoine Pogba alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu kabla ya kukumbwa na mauti hayo familia ya Pogba imethibisha kutokea kifo hicho katiak hospitali ya Le Parisien.
Fassou mwenye asili ya Guinea alihamia Paris, Ufaransa miaka 30 iliyopita nchi ambayo Paul anaichezea katika mashindano ya kimataifa.
Watoto wake wengine ni mapacha Florentin na Mathias wenyewe wameamua kucheza nchi anayotokea baba yao Fassou.
Fassou alipiga picha akiwa jukwaani wakati wa fainali ya Euro 2016 zilizofanyika Ufaransa, akiwa na Florentin na Mathias washangilia Paul akichezea Ufaransa dhidi ya Uswisi.
USISAHAU KUTUFATILIA KUPITIA
No comments:
Post a Comment