KARIBU YAKO ZAIDI

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

May 24, 2017

Mambo Ya Kuzingatia Katika Biashara

Yamkini unataka kufanya biashara, au umekwishanza kufanya ila katika biashara unayofanya mara nyingi huoni matokeo ambayo ulikuwa unategemea. Hii ni kutoka unafananya au ulifanya biashara kwa kutokufanya uchunguzi wa kina juu ya biashara hiyo.

Unajua ni kwanini biashara yako haisongi mbele? Shusha pumzi kisha twende sawa kwani leo ndio siku ya pekee kwako kuweza kuona unapata faida endapo utaisoma Makala hii kwa umakini na kuielewa kisha kuiweka katika matendo, kwani inawezekana ukawa ni mfuatiliaji mzuri lakini sio mtendaji mzuri ila nikuombe tena kwa mara nyingine utakachokisoma hapa kiweke katika matendo na utakwenda kuona matokeo yake.

Yafuatayo ndiyo mambo ya kuzingatia katika biashara.

1. Elewa biashara yako vizuri.
Mara nyingi inawezakana unashindwa kuona unapata mafanikio hii ni kwa sababu hauifamu biashara yako vizuri. Inawezekana ukawa haujanielewa twende sawa, kuifamu biashara hapa nina maana ya kwamba watu wengi tunafanya biashara kutokana na kusikia kwa watu ambao wamesema kuwa biashara fulani inalipa, na baada ya kusikia hayo unakwenda moja kwa moja kwenda kuifanya matokeo yake biashara hiyo inakufa. Hii unajua ni kwanini ni kutokana na hukufanya utafiti wa kutosha juu biashara hiyo.

Inawezekana kweli biashara fulani ikawa inalipa na wewe ukagundua hilo jambo la msingi jaribu kuchunguza ni mbinu zipi ambazo wanazutumia mpaka waseme hivyo.

Pia ukumbuke ya kwamba kusikia peke yake haitoshi, moja ya sifa kubwa ya mjasiliamali ni lazima ajue kufanya uchunguzi wa kutosha wa jambo lolote kabla hajaanza kulifanya. Wito wangu kwako Ni kwamba itambue biashara yako vizuri hii itakusaidia kujua changamoto na jinsi ya kukabiliana nazo. Kuna mwandishi mmoja aliwahi kuandika ya kwamba usiishie kusema ndoto yangu ni kuwa hivi na vile bali anza kufanya sasa, ndoto hiyo kuwa kweli. Amini ya kwamba unaweza kuifanya ndoto kuwa kweli ndani ya muda mfupi.

2. Simamia na thibiti biashara yako.
Hili jambo la msingi zaidi kuliko hata kula anashangaa! Usishangae wala hujakosea kusoma upo sawa kabisa. Unajua kwa nini nimesema hivyo watu wengi biashara nyingi hazina Maisha marefu hii ni kutoka hatuna usimamizi wa mzuri wa shughuli zetu. Tupo baadhi yetu tunaendesha biashara kubwa ambazo kwa siku zinaingiza pesa nyingi kwa kuwa tunakwepa kuwalipa wafanyakazi mishara mikubwa tunajikuta tunawatafuta watu wanyonge wawe wasimamizi wa biashara hizo na kuwalipa mishara midogo na kwa kuwa wafanyakazi hao wanajua wewe bosi unaingiza shilingi ngapi mwisho wa siku wanaona unawalipa mishara midogo wanaanza kukuibia.

Kitu cha msingi ni kwamba jaribu kuwajenga wafanyakazi wako waione biashara yako ni sehemu ya maisha yao. Wapo baadhi ya wafanyakazi katika biashara endapo atanunua hata nguo mpya bosi wake humuuliza hiyo nguo umeitoa wapi unashangaa huo ndio ukweli, wewe bosi ukiishi katika misingi hiyo ni lazima utaibiwa tu kila siku na biashara yako haitakuwa ikisonga mbele maana kila mfanyakazi unayemuajiri utamuona jipu tu.

Kumbuka ya kwamba kuwa biashara yako inaweza kukua kwa kumfanya mfanyakazi kwa kumfundisha mambo ambayo yataijenga biashara yako. Mfundishe mfanyakzi wako kuweza kuongea vizuri na wateja, mfundishe kuandika kumbukumbu kwa kila mzigo unao ingia na kutoka hii itakusaidi sana pia na wewe bosi ni lazima uwe daftari ya tarifa ya kumbukumbu tofauti na wafanyakazi wako.

Moja ya sababu inayopelekea biashara nyingi kufa ni kule kutokuwa na mahusiano mazuri baina ya mwajiri na mfanyakazi. Wito wangu kwako mfanyakazi ipende kazi yako kuwa mbunifu kwa kumshauri mwajiri wako mbinu kadha wa kadha katika kupanua soko. Na wewe mwajiri Kuwa na mahusiano mazuri na mfanyakazi usimuone eti kwa sababu hana pesa na elimu ya kutosha kama wewe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages