Timu ya VIONGOZI wa serikali chini ya uongozi wa kocha mchezaji Mkuu wa Mkoa wa Mbeya imeibamiza bila huruma timu ya VIONGOZI wa DINI mabao 4-1
Mpira ulikuwa mkali ila timu ya VIONGOZI wa serikali iilionekana kucheza kwa maelewano hivyo kuisaidia timu hiyo kuibuka mshindi na kumaliza tambo za muda mrefu za timu hizo angalia matukio katika picha hapa chini
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla akikokota mpira mbele ya mchezaji wa timu ya viongozi wa dini katika mchezo uliofanyika leo kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku viongozi Timu ya viongozi wa Serikali ikitoka kifua mbele kwa kushinda magoli 4-1 dhidi ya timu ya viongozi wa dini.
Wachezaji wa timu za viongozi wa Dini na Viongozi wa Serikali zikichuana vikali kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika leo.
Mchezaji wa timu ya Viongozi Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla akinyanyua juu kombe waliloshinda dhidi ya timu ya viongozi wa Dini katika mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine.
Mchezaji wa timu ya viongozi wa serikali na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo kwye uwanja wa Sokoine ambapo timu yake imeifunga timu ay viongozi wa dini magoli 4-1.
Timu ya viongozi wa dini ikikaguliwa na mgeni rasmi kabla ya kuanza kwa mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
No comments:
Post a Comment