Rapa huyo amewashukuru mashabiki wake kwa ushirikiano waliomwonyesha katika project yake ya wimbo ‘Muziki’.
“Good morning from Bongo Tanzania East Africa to the Top of the world!. Nataka kusema asanteni sana kwa love na support ambayo mmetupatia kwenye project yetu ya ‘Muziki’ na kuipelekea kuwa National Anthem. Hakuna neno linaweza kumaanisha thamani yenu kwetu! God bless you all usikose kusikiliza project yetu mpya leo #CMG#HasarARoho,” aliandika rapa huyo Instagram.
Mmoja kati ya mameneja ambao wafanya kazi na rapa huyo, Hanscana, hivi karibuni aliiambia Bongo5 kuwa ujio mpya wa rapa huyo umeandaliwa kama anavyoandaliwa mtu anayekuja kuwa Rais wa nchi.
“Sisi tumejiandaa vizuri kwa sababu tunajua mashabiki wanataka nini. Maandalizi ni makubwa sana, yaani ni kama tunaandaa Marais 5 wa nchi. Kwahiyo tumejipanga vizuri kuhakikisha jamaa anarudi vizuri katika game,”
Video ya wimbo ‘Muziki’ wa rapa huyo imeangaliwa mara 7,056,225 kwa kipindi cha miezi 5 tu.
No comments:
Post a Comment