KARIBU YAKO ZAIDI

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

May 4, 2017

Mbeya City tayari kuikabili Yanga


Kikosi cha Mbeya City kimerejea jijini Mbeya, baada ya kumaliza kambi yao mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, ambayo ikiwa na lengo la kujiandaa kuwakabili Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.
Kikosi cha Mbeya City kiliweka kambi mjini Sumbawanga, ikiwa ni sehemu ya mapendekezo yaliyotolewa na uongozi wa benchi la ufundi chini ya kocha kutoka Malawi, Kinnah Phiri ili kujifua kwa mechi zijazo za kumaliza msimu huu.
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Mbeya City, Dismas Ten, amesema dhumuni kubwa la kuweka kambi mjini Sumbawanga lilikua ni kufanya maandalizi ambayo yataendana na hali ya hewa ya jiji la Dar es salaam, ambapo ndipo watakapocheza dhidi ya Yanga Mei 14.
Tunaamini maamuzi yetu ya kwenda Sumbawanga yalikua sahihi na tumefanikiwa kucheza michezo minne ya kirafiki ambayo itatusaidia kufanya vizuri katika mchezo wetu dhidi ya Yanga. Tunajua mchezo utakua mgumu na ndio maana kocha wetu ameamua kuutumia vizuri muda huu wa mapumziko ya ligi, ili kupata kambi ya muda mrefu sambamba na kucheza michezo ya kirafiki.”Alisema Dismas Ten kwenye mahojiano yake na Times FM.
Mbeya City ilikabiliwa na matokeo mabovu katika michezo minne waliyocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Kumbukumbu Ya Sokoine Jijini Mbeya, hali ambayo ilizua taharuki kwa mashabiki wao na kufikia hatua ya kuutaka uongozi wa juu kuwatimua wahusika wa benchi la ufundi.
Mbeya City itavaana na Klabu ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara kunako Dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaaam,Tarehe 14 mwezi May mwaka huu.
By Godfrey Mgallah

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages