Katibu NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Humphrey Polepole Akimkabidhi cheti mmoja wa wanachama Ndugu Juma Toka SAUT-ARUSHA |
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Vyuo na Vyuo Vikuu katika Mkoa wa Arusha umekuwa na ugeni wa Katibu NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Humphrey Polepole ambaye amekuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Vijana wa CCM Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Arusha .
Katika hatua nyingine ndugu Humphrey Polepole ametoa Vyeti kwa Wahitimu 268 na kupokea Wanachama Wapya wa CCM zaidi ya 65 na Kuwapa Kadi za Uanachama na kisha kuwaongoza kula kiapo cha uaminifu ndani ya CCM. Mahafali yaliyoudhuriwa na Wanachama 523.
No comments:
Post a Comment