Mtanzania anaejulika katika mitandao ya kjamii kwa mbwembwe za kutumia pesa, Jack Pemba, amejikuta akiwa katika selo za nchini Uganda kwa kosa la kutakatisha pesa.
Msemaji wa jeshi la Polisi Nchini Uganda, Asan Kasingye, amesema kuwa Jack Pemba amekamatwa, na kuongeza, wakati akitaka kukamatwa, alijaribu kutoroka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe.
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Monitoring, inadaiwa kuwa kulisambazwa kwa picha zikimuonesha Mtanzania huyo anayeishi Uganda akigawa pesa katika matamasha ya muziki, na hivyo kutiliwa shaka juu ya chanzo cha utajiri wake.
Hivi karibuni Jack anadaiwa kuhusika katika sakata la wizi wa madini ya dhahabu yenye thamani ya Shs Bilioni 25
No comments:
Post a Comment