KARIBU YAKO ZAIDI

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

May 3, 2017

Muntari apewa adhabu baada ya kuondoka uwanjani kwa hiari

Kiungo wa kati, Pascara Sulley Muntari, amepewa adhabu ya Mechi moja baada ya kutoka ndani ya uwanja bila ya kutolewa na hivyo kuigharimu timu yake kucheza kwa upungufu uwanjani, huku Mchezaji huyo akilalamikia matamshi ya kibaguzi yalio kuwa yakitolewa uwanjani hapo dhidi ya mashabiki wa timu pinzani.
Alipewa kadi ya manjano katika Mchezo huo baada ya kumuomba refa asimamishe mechi siku ya Jumapili dhidi ya Cagliari akisema kuwa alikuwa akibaguliwa kwa misingi ya rangi yake.
Mchezaji huyo wa zamani wa Ghana mweye umri wa miaka 32, aliamua kutoka uwanjani, hatua iliyosababisha apewe kadi ya pili ya manjano.
Maafisa wamesema kuwa, sio mashabiki wengi waliosikika wakitoa maneno ya ubaguzi kuweza kusababisha hadi kuchukua hatua.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages